Huduma ya Upatikanaji wa Asali (Misitu Honey)

Utangulizi

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania umepewa majukumu ya  Kuanzisha na kusimamia Hifadhi za Nyuki  na Manzuki za Serikali kuu. kufanya biashara ya mazao ya ufugaji nyuki  na huduma. Aidha, Wakala unasimamia utekelezaji wa sheria ya Ufugaji nyuki, ikiwa ni pamoja na kutoza tozo  na ada mbalimbali za mazao ya nyuki kwa mujibu wa Tangazo la serikali namba (GN) 454 la mwaka 2019. Kwa mujibu wa Tangazo hilo asali inapatikana kwa shilingi 10,000 kwa kilo.

Wakala unazalisha na kuuza asali yenye chapa ijulikanayo kama  “MISITU HONEY”, chapa hii ina sifa ya kuzalishwa kutoka kwenye mchananyiko wa miti ya Maua yaliyopo kwenye Hifadhi za Misitu na Hifadhi za Nyuki zinasosimamiwa kwa misingi endelevu. Aidha, MISITU HONEY inachujwa na kufungashwa katika hali ya usafi wa hali ya juu katika viwanda vya kuchakata asali vya Manyoni, Saohill na Tabora. Asali hii imesajiliwa na kupewa alama ya Ubora na Shirika la viwango Tanzania (TBS).

MISITU HONEY limesajiliwa na Msajili wa Makampuni na Majina ya Biashara (BRELA) kwa usajili namba TZ/T/2020/000621.

Asali hii inapatikana katika maduka rasmi ya asali, ambayo Duka la Asali Mpingo House, Mkoa wa Dar Es Salaam, Manyoni, Mkao wa Singida, Sao Hill Mkoa wa Mafinga na Duka la asali Ofisi za TFS Kanda ya Kati. Vilevile MISITU HONEY inapatikana katika Ofisi ya TFS kanda ya Kaskazini, Kanda ya  Ziwa na Kanda ya Kusini.

Namna ya kununua Asali ya Misitu

Huduma ya kununua asali ya MISITU inapatikana kwa kutumia mfumo wa kieletroniki wa malipo ya Serikali, kupitia kupatiwa kumbukumbu ya namba ya malipo inayoandaliwa kwa mteja na kulipwa kwa njia ya simu kupitia mitandao ya M- Pesa, Tigo Pesa, AIRTEL Money, Halopesa na TTCL PESA au kuskani QE CODE kwa kuchanja kwa kadi ya Benki.

Hatua za kulipia kupitia mtandao wa VODACOM.
PIGA *150*00#

  • 4 Lipa kwa M-Pesa
  • 5 Malipo ya serikali
  • 1 namba ya Malipo
  • Ingiza namba ya malipo
  • Ingiza kumbukumbu namba
  • Ingiza namba ya siri kulipia

Hatua za kulipia kupitia mtandao wa TIGO
PIGA *150*01#

  • 4 Lipa Bill
  • 5 Malipo ya serikali
  • Ingiza kumbukumbu namba
  • Ingiza namba ya siri kulipia

Hatua za kulipia kupitia mtandao wa TTCL
PIGA *150*71#

  • 5 Lipia Bill
  • 3 Malipo ya serikali
  • ingiza kumbukumbu namba
  • Lipia Bili
  • Ingiza kiasi
  • Ingiza namba ya siri kukamilisha malipo

Hatua za kulipia kupitia mtandao wa HALOTEL
PIGA *150*88#

  • 5 Lipa kwa Halo pesa
  • 7 Malipo ya serikali
  • Ingiza kumbukumbu namba
  • Ingiza kiasi
  • Ingiza namba ya siri kulipia

Hatua za kulipia kupitia mtandao wa AIRTEL
PIGA *150*60#

  • 4 Lipa Bill
  • 5 Malipo ya serikali
  • Ingiza kumbukumbu namba
  • Ingiza kiasi
  • Ingiza namba ya siri kulipia